News, Advertisements & Business
At least 1 million passengers have traveled aboard the standard gauge railway (SGR) electric trains between Dar es Salaam, Morogoro, and Dodoma, the capital of Tanzania, since the service's launch...readmore
Simba sports club silence CS Constantine to top Group in CAF confideration Cup.
Kimbisa: President Samia, Dr. Mwinyi should be given the opportunity to run in 2025....readmore
Watahiniwa 477,262 Kati ya 516,695 waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2024 wamefaulu kwa 92.37% ,ukilinganisha na matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2023 ambapo watahiniwa waliofaulu walikuwa 471,427 sawa na 89.36%, ambapo kati yao wasichana ni 249,078 sawa na 91.72 na wavulana 228,184 sawa na 93.08%.
Pia Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA) Dkt. Said Mohammed amesema ufaulu wa somo la Basic Mathematics kwa kidato cha nne bado upo chini ya wastani licha ya kuendelea kuimarika kwa miaka 10 hivyo juhudi za ziada zinatakiwa kuongezwa kwenye somo hilo.
The National Examination Council of Tanzania release SFNA results 2024/2025...readmore
AFYA: Januari 20, 2025, Serikali ilitangaza mlipuko wa Ugonjwa wa Virusi vya #Marburg (MVD) katika Wilaya ya Biharamulo, Mkoani Kagera baada ya Mtu mmoja kukutwa na Maambukizi.
Kufuatia taarifa ya mlipuko wa Ugonjwa huo, Serikali imetoa mwongozo wa Wasafiri wanaoingia na kutoka Mkoani Kagera kwa kuandaa Ushauri wa Usafiri Na. 15 Januari 21, 2025 ili kudhibiti usambazaji na ueneaji wa Ugonjwa huo Nchini.
MAREKANI: Mwanamuziki Chris Brown amewasilisha kesi dhidi ya Kampuni ya filamu, Warner Bros. Discovery, akiidai Kampuni hiyo kiasi cha Tsh. Trilioni 1.2, akidai kwamba Kampuni hiyo imechapisha taarifa za uongo na zinazomdhalilisha kupitia 'Documentary' ya "Chris Brown: A History of Violence" .
Mwanasheria wa Chris, Levi McCathern amesema "Kesi hii ni kuhusu kulinda ukweli, licha ya kupewa ushahidi kuwa taarifa hizo si za kweli bado Kampuni hiyo iliandaa 'documentary' hiyo na kuichapisha kwa makusudi wakifahamu wako kinyume na majukumu yao kama Waandishi wa Habari."
#HABARI Kufuatia tukio la wavuvi zaidi ya 500 waishio katika kijiji cha Nankanga, kuzama kwenye maji baada ya mitumbwi yao kulemewa na upepo uliotokana na dhiruba kali katika Ziwa Rukwa wakati wanatekeleza majukumu yao,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Helikopta ya jeshi iliyoambatana na wazamiaji na vifaa maalum vya uokozi ili kuongeza nguvu ya uokozi .
Tayari Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, Januari 24, 2025 alifika kwenye kijiji hicho kuungana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Dkt. Ashatu Kijaji kujionea hali ya uokozi inayoendelea ambapo mpaka sasa wavuvi 540 wameokolewa na wengine 10 wanatafutwa.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Nyakia Chirukile ameeleza kuwa mnamo Januari 23, 2025, jumla ya wavuvi 550 kutoka Kata ya Nankanga na Mtowisa waliokuwa wanaendelea na shughuli za uvuvi kwenye Ziwa Rukwa walipatwa na dhoruba kali ya upepo ulioikumba mitumbwi yao, na kisha kuzamishwa, ambapo kufikia siku ya Jumamosi Januari 25, 2025 jitihada mbalimbali za kuokoa zinaendelea kufanywa na wananchi kwa kushirikiana na Jeshi la Uokoaji ikiwa ni pamoja na kuwatambua wavuvi ambao walikuwa hawajasajiliwa...readmore